Share this:

MWONGOZO WA KIDAGAA KIMEMWOZEA.

KIDAGAAA KIMEMWOZEA

-UTANGULIZI

 

“Kidagaa Kimemwozea” ni kitabu chenye jalada jeusi iliyorembeshwa kwa picha ya mwanamwali mmoja mrembo aliyekuwa akidondoshwa na machozi. Riwaya hii ni aina ya kipekee,inayothibitisha usanii wa kupigiwa mfano jinsi ndoto ya uhuru barani Afrika ilivyogeuka kuwa jinamizi inayowafanya wazalendo kulia, “kidagaa kimetuozea” kwa kutamaushwa na usaliti wa viongozi wa baada ya Uhuru.

Hapa twafahamu kuwa kidagaa kilichokuwa kimeoza kiliwaozea wanyonge haswa, kwa kupitia wahusika kama Amani, Imani, Uhuru, DJ, Matuko n.k. wahusika hawa pamoja na wengine ndio wale wanaodhulumiwa na viongozi wao ambao, badala ya kuonyesha uongozi mwema, wanaongoza kwa kuwatesa na kuwanyang’anya na hata kuwaua wananchi wanaofaa kuwalinda. Hadithi hii imetolewa kupitia safari ya wahusika wawili, Amani na Imani. Wawili hawa

wanang’oa nanga kutoka mastakimunini mwao kuelekea mji wa Sokomoko ili kutafuta kazi zitakazowafanya kuishi maisha ya faraja na yenye buheri wa afya.

Hata hivyo katika safari yao, wanafika ukingoni mwa mto Kiberenge ambao maji yake yanasitishwa na wenyeji kwa tuhuma kuwa ni maji ya kifo. Amani na Imani wanavunja mwiko huu kwa kuyanywa maji haya. Tendo hili ambalo Imani anadai kuwa ni kuhalilisha yaliyo haramu linawashangaza wenyeji ambao kwa kuogofya matokeo yake, wanagundua kuwa waili hawa hawaathiriki kivyovyote vile.

Msimulizi anapata nafasi nyingine ya kuendeleza masimulizi yake kupitia mto Kiberenge. Kupitia chombo hiki cha mto Kiberenge, msomaji anagundua kwamba ni wale tu wataoyanywa maji haya yaliyo haramu, ndio wanaoweza kuendeleza vita vya kupatia Uhuru.

Hili linatimika kwa sababu, mara tu Amani na Imani wanapofika tu Sokomoko, wanaajiriwa na ndugu wawili, Mtemi Nasaba Bora na Mwalimu Majisifu ambao wote ni wanyanyasaji.

Kupitia Nasaba Bora, Mwalimu Walibora andhihirisha kuhusu mizozo ya ardhi baada ya Uhuru ambapowanyonge wananyang’anywa mali na mshamba yao kunyakuliwa. Wachochole wananyang’anywa mashamba yao na Mtemi Nasaba na aina yake ambao pia wanatumia vibaya nafasi za uongozi.

Kwingineko, mwandishi anamdhihirisha Majisifu kuwa tapeli aalimu anayewaibia watu miswada yao. Anapokadhibiwa maandishi na wachapishaji wanaomtarajia kuyachambua na kasha kuandika ripoti, anatenda kinyume kwa kuandika ripoti mbovu na kasha hatimaye, kutumia mawazo yao kujiendeleza kiunafiki.

Hili linadhihirisha wazi maovu katika Nyanja za elimu ambapo wanagenzi wetu hutapeliwa ugwiji wao na wale wanaofaa kuwaendeleza.

Hata hivo, Amani na Imani wanapigania vita vikali dhidi ya maovu katika jamii baada ya kugundua haki zao. Wanaongoza umati ulio na kiu ya kupata ardhi zao zilizonyakuliwa na Mtemi Nasaba na aina yake. Wanaongoza kikosi takatifu pamoja na wale walio na mawazo kama hayo. Kikosi hiki kinaweza kuwakilisha mabadiliko ya uongozi baada ya Uhuru katika mataifa ya Afrika ambapo hali ya ukosefu wa maendeleo itasitishwa.

Riwaya hii bila shaka itawa wa umuhimu kwa wanafunzi wa shule za upili na vyuo vikuu. Kando na kazi za awali za Walibora, Kidagaa Kimemwozea inajumuisha utajiri wa usanii, hali kadhalika misemo. Kazi yenyewe kwa kweli inajumuisha vyombo tofauti tofauti vya usanii kama, hadithi ndani ya hadithi,visakale, visaawali na mengineyo, yaliyojumuishwa miongoni mwa waandishi wa riwaya wenye tajriba za juu yalichapishwa hivi majuzi katika nchi za Afrika Mashariki.

ecolebooks.com

 

SURA YA KWANZA

Chini ya mti mmoja kando yam to Kiberenge, vijana wawili, amani na Imani wanapunga hewa baada ya kukata kiu. Aidha, wamo safarini kuelekea Sokomoko, kila mmoja na haja yake.

Kitambo kidogo tu, wawili hawa wamevunja mwiko kwa kuyanywa maji yam to kiberenge ambao wenyeji wanaamini kuwa haramu.

Muda si kitambo, wenyeji hawachelewi kuambizana na kusimuliana juu ya waja wawili, waliovunja mwiko kwa kuyanywa maji haramu ya Kiberenge na wakakosa kuaga dunia. Kwa kweli, wakati mwingine haramu huweza kuhalalishwa kulingana na watendwa. Imani anayo imani kwamba hakuna haja yoyote ya kuogopa kutenda bila kujaribu.

Ni katika harajkati hizi za kukata kiu ndipo wanapokutana na vijana wanaokoga na kupiga mbizi mtoni. Wakti huu,mifugo ya matajiri wanala nyasi baada ya kujitosheleza kwa maji.

Fahali mmoja mweusi anaizoa kinywani suruali moja kuukuu linalomilikiwa na na kijana mmmoja mneni sana. Wanapogundua linalojiri baada ya kufahamishwa na Imani, vijana wale wanaparamia ukingoni na kuanza kumfukuza Yule fahali lakini wapi, anaposimama, suruali keshaimeza tumboni.

Ndilo vazi la kipekee alilokuwa nayo DJ, kwikwikwi na msononeko zikamkaba yule kijana hohehahe asiye na mbele wala nyuma. Jahazi linaokolewa na Amani anapofungua mkoba wake na kutoa shati moja, akamwita kijana yule na kumpoza shati.

Kwa kuwaamini wageni hawa wasiojulikana kutoka kwao, DJ anawasimulia yaliyomjiri. Kazaliwa na kukuzwa na mama mmoja mpishi wa pombe haramu mtaani Madongoporomoka mjini Songoa. Kasingiziwa kuiba na kufungwa jela ya watoto anakotoroka na ndipo kufika Sokomoko anakoajiriwa na mkewe Maozi kama mmoja wa familia.

Hatimaye, wanaandamana kuelekea Sokomoko ambako DJ awaelekeza kwa ndugu wawili matajiri, Mtemi Nasaba Bora anayehitaji mchungaji ilhali kakake Mwalimu Majisifu anahitaji kijakazi. Njiani, anawatahadharisha kuhusu udhalilishaji na mishahara duni ambazo wangekumbana nazo.

Hapa ndipo Amani kategua siri kadhaa zikiwemo kutafuta njia yakumwokoa amu yake na kufichwa kwa mali ya nasaba yake. Kajitayarisha kukumbana na mahasimu wake, bila dhamira ya kulipiza kisasi. Imani naye kafika kwa kukosa pa kuenda baada ya mastakimu yake kuteketezwa na wasiojulikana. Amani ana umri wa miaka ishirini naye Imani kumi na minne. SURA YA PILI

Eneo la Sokomoko ambako ni kwa matajiri. Kitambo kabla ya Uhuru, eneo hili lilikuwa limetengewa Wazungu pekee. Wamiliki walipanda mimea tofauti tofauti ikiwemo pareto, alizeti na kadhalika. Weusi hawakuruhusiwa kuishi wala kulima mazao yoyote yaletayo fedha. Mweusi angefuga tu mifugo ya kienyeji lakini njee ya Sokomoko.

Matajiri wa Sokomoko waliyanyaka ardhi zile zilimilikiwa na wakoloni ambao walirudi makwao. Miongoni mwa Wazungu hao, Major noon almaarufu Majujnuni ambaye shamba lake lilinyakuliwa na Nasaba Bora, kaacha nyuma kasri moja kubwa alililokuwa amejengea mpenziwe Michele ili wakaishi pamoja.

Mara yake ya kwanza kuja Afrika baada ya vita vya pili vya dunia, Majununi kajenga hema na kasha kumwalika mpenziwe Michele. Kidosho huyo kafika, akakataa katakata kushuka toka kwenye ndege na kumwambia Majununi kwamba hawezi katu kuishi mwituni kama mnyama. Akaabiri ndege na kurudi kwao Ufaransa. Kujenga nyumba yenye viumba vinne, Michele kanengua kuwaq kamwe hawezi kuishi ndani ya kibanda. Majununi akawa mtaftaji asiyechoka, ila akichoka, basi huwa keshapata. Kajenga basi kasri kubwa lenye viumba kumi na vitatu. Asiyetosheka na la ninaye, kumbe la mweziwe maradhi. Mara hii, kidosho kashuka na kuingia mle kwenye kasri, vyumba kumi na vitatu? Bahati mbaya. Sakafu yenye rangi nyekundu? Hatari, na mbona madirisha makubwa.

“Monsieur Noon, naomba radhi sana lakini hatufaani. Pengine imeandikwa kwamba tusioane. Narudi kwetu. Katafute mwanamke kufu yako.” Ndiyo maneno yake Michele kabla ya kuabiri ndege na kurudi kwao.

Akakosa hata tone moja la mahaba rohoni kwa wanawake wote Majununi, na kasha kaingilia ukulima na ufugaji kwa moyo, acha roho. Hata hivyo kwenye bamba la zege karibu na dohani ukumbizoni kaandika, “Your beauty is my weakness”, maneno yaliyobaki kuwa ukumbusho

kwake kuhusu mapenzi yake kwa Michele.

Mteni Nasaba akiwa kwenye Wizara ya Ardhi kajitengenezea stakabadhi alizozitumia kunyakua shamba la mwajiri wake. Akawa Mtemi, mkubwa, nusu mungu sijui nini. Watu wakawa ni kufyata ndimi dhidi ya dhulma zake Mtemi. Akawa wa kuvunja wale waliodhubutu kumpinga na kuckichukua akitakacho. Kwake hoja ikawa kupata alichokitafuta, wala si jinsi ya kukipata. Kwake Mtemi usafi zaidi kukawa balaa. Vitu vikuukuu, hela hatumii hajali. Machweo wakafika akina Amani kwa Mtemi. Wakampata kamsimamia fundu aliyekuwa akibambanyabambanya katika injini. Kawatupia jicho la dharau na kuwauliza maswali za upumbavu. Akawakodolea macho na kushangazwa na jawabuye Imani, aliyemtizama kwa kumkazia macho Mtemi havumilii. “Usinivue nguo kwa macho yako wee!” (uk 21).

Akawaaga baada ya kumsukuma kidogo, eti aenda “kusukuhisha mgogoro wa shamba…” (uk

21). Akatokomea hukoo!

Basi DJ kamfikisha Amani kwa Bi Zuhura, mkewe Mtemi Nasaba Bora. Amani akawa akisubiri kuonyeshwa makazi yake, kwenye kibanda la wafanyikazi, la makabwela kama yeye. Kufuka nje kwa Imani na DJ, jibwa lile jeupe, aliyedhoofika na kung’ookang’ooka ngozi haliachi “kubweka bwe bwe, bweka ubweke kufa kwaja.” (uk 24) akamwonea huruma DJ na kuuliza kwa nini kwa nini lisiachwe “free maze”.

Akakumbushwa na Bi Zuhura asiwe “kama wazungu wanaopaswa kukumbushwa kwamba mbwa ni ni mnyama”. Kukawa tayari kumeingia machweo walipotoka akina DJ.

SURA YA TATU

AMANI NA Imani wakaangukia kazi duni zisizotamanika, mishahara duni sisemi. La kulalamika hawana, wakubali wametosheka, kwani kunao wasio hata na ajira yoyote. “Tukilalamika hatua viatu tutaambiwa wapo wengine hawana miguu”. (uk 25)

Amani kaajiriwa uchunga na Mtemi Nasaba bora na Imani kujisitirisha kwa Majisifu, matajiri wawili, ndugu wasiopikika chungu kimoja kama chui na mbuzi. (uk 25) Mwalimu Majisifu akawa wa kusifika kote nchini na kujulikana hata na wasiojua kusoma. Aha! Usisahau kumwiga. Akatunga nyimbo zilizombwa katika sherehe nchini Tomoko. Haya yote yatokana na kuandika kwake kwa kitabu chenye anwani “Kidagaa kimemwozea”. Hata hivyo juu ya sifa hizo zote, akawa tu mwalimu wa shule ya upili ya Nasaba Bora.

Majisifu kaelimishwa na misheni kama nduguye mkubwa. Akaenda ughaibuni alikorudi na shahada mbili za digrii na miwani,elimu yake isiyofikiwa kiwango na wengi wa Wanasokomoko. Kwake anayo nafasi za kazi kiganjani, “…hakutafuta kazi, zilimtafuta”. (uk 28)

Akabadilisha dini na kuabudu pombe. “Pombe ilikuwa mungu wake na ulevi ndio ibada aliyoipenda kwa dhati…” (uk 28) Akavuliwa mbeleko, ..akapewa ualimu wa kufutia machozi…” (uk 28) Kwake Majisifu kukawa na kila aina ya viombo na vinywaji kutoka mataifa mbalimbali. Hata hivyo, kipi kilicho kizuri kisichokuwa na ubaya wake? “Majisifu hakuwa mgumba wala mkewe Dira hakuwa tasa.” (uk 30)wakawazaa watoto, mapacha mapacha, wenye ulema uiokithiri. Wanao wawili, msichana umri miaka kumi na saba naye mvulana kumi na sita, haja ndogo na kubwa wanaenda kwenye mavazi. Utajiri aliokuwa nao babao hawajui, hawajielewi watokako au waendako. Akajiona wa laana majisifu, akasusia kumjua mkewe karibu kumi na mitano miaka.

Siku moja kazidiwa na kumpenda mkewe. Wakabahatika mapacha, hawa nao hawatembei. Akatamani kuwatupa majini akazuiliwa na Dora. Hata hivyo, majisifu hakukawia kuwaonea gere waja wote. Kajitokeza imani na kuvunja mwiko wa pili, “…aliwapenda wale watoto walemavu kwa dhati…” (uk 31)

Amani akapolea kibandani kwake, kuliko tu na wendani wa karibu, “jeshi kubwa la mijipanya…” (uk 32) asiwe na chochote cha maana. Ukutani Amani katundika mkobake kilichobeba nguo zake na picha ya amu yake yusufu, ambaye ala kalenda kwa tuhuma za kumwua babake, “Chichiri Hamadi, ambaye alikuwa na shamba kubwa huko Sokomoko alilopokonywa…” (uk 33). Amani na mamake wakahamia Ulitima. “La mama mtu hakuwa mkwasi wa kutajika bali pia hakuwa maskini mwenye hali ya mkunga, akijikuna hutoka unga”. (uk 33) Akaaga dunia

mwanaye amani akiwa na umri wa miaka ishirini.

Alfajiri moja, Amani kagutushwa kutoka lpe la usingizi na usiahi mkali mlangoni pake. Alipochungulia, kampata motto mmoja, umri siku moja hajatimiza. “Akatekwa hajui afanyaje” (uk 35). Akakionea kite kile kitoto na kumchukua kibandani mwake. Kulipopambazuka, akakibeba na kuelekea kwa Mtemi. Akakaribishwa na Bi Zuhura, acha Mtemi aingie. Bi Zuhura akashtuka, “…kilifanana na mtu fulani pale kwenye kasri la Majununi” (uk 39). Tusisahau kwamba Mtemi karejea jogoo la kwanza toka alikoenda “kusuluhisha mgogoro wa shamba.” (uk 39).

Akaingia ukumbini Mtemi na “kukikodolea macho kile kitoto kilichopakatwa”. (uk 40) Akatoa uamuzi kwamba Amani akamchukue mwanawe na kumlea. Kwa sababu Mtemi ni mkubwa, hakuna athubutiaye kumpinga. “Ulikuwa uamuzi wa haki, na uamuzi wa haki haubatilishwi.” (uk

41) Akambeba mwanawe wa kupagazwa na kurudi kibandani.

Muda si mrefu, akamwona DJ na kumwita. Akamweleza yaliyotukia na kumtuma DJ akamweleze Imani kilichokuwa kikijiri. Naye Imani kawa mja wa kuelewa, akatoka asubuhi hiyo na kuelekea kibanda cha Amani.

Wakti ambao haya yanaendelea, bintiye Maozi, Lowela hayuko hapatikani. Amani akawaza na kukumbuka kisa cha mwandani wake Fao ambaye kampachika mimba mwafunzi mmoja na kasha kutokomea ughaibuni. Mengi, kajisomee wewe katika kurasa 35-37.

SURA YA NNE

“Siku tatu tangu Imani kende kwa nduguye nab ado hajaonekana.” (uk 49) Dora hakuweza kuvumilia kuwa linda wanawe. Akazidiwa hamaki na kumshambulia mumewe Bwana Majisifu ambaye kajibu kwa “kumfungulia cherehani ya matusi” (uk 52).

Hata hivyo, majibizano hayo yanakatizwa ghafla mlango unapobishwa na mpwa wake majisifu, Mashaka bintiye Mtemi Nasaba Bora. Majisifu na Dora wanavua nyuso za hasira na kujibandika za bashasha, anagalau mgeni asijejua siri za jirani. Haisuru, wanaingia katka gumzo, ambapo Mwalimu Majisfu hachoki kumkosoa Mashaka.

Baada ya Dora na Mashaka kujiburudisha kwa chai, iliyosusiwa na Majisifu, kwani siku hizi kakosa tumbo la kuikarisha, sababu yenyewe keshazoea sharabu. Ndipo Mwalimu Majisifu anamwuliza mpwake kazi ambayo angependa kufanya baadaya ya masomo. “Napenda niwe mwandishi wa vitabu kama wewe amu”, (uk 47) akajibu Mashaka. Kwa kumalizia, Majisifu akaboronga lugha, “Kitanda usichokilalia hukijui kunguni wake” (uk 47).

Acha mashaka aulizie muda aliouchukua mwalimu Majisifu kukiandika kitabu chake cha “Kidagaa Kimemwozea”, jawabu likawa kaski mosi. “Aha, kurasa zote hizo?” akaendeleza mashaka. “Mwandishi bora lazima aandike haraka kabla mwazo hayajayeyuka kuwa upepo (uk

48).

Anapoondoka Mashaka, anampasa Mwalimu Majisifu barua inayomwalika Wangwani ili kutoa mihadhara kuhusu uandishi wake. Anamfahamisha Dora ambaye baada ya kuomba kuletewa “rinda na viatu toka Mkokotoni”, anaanza tena kushambuliana. “Kama utaweza, mbwa apige mswaki.” (uk 51). Anaghadhabika Mwalimu na kijibu kwa matusi. Hata hivyo tunajulishwa kwamba “nyoko nyoko” zilikuwa shibe za kawaida kwao.

Amani na Imani wanastakimu pamoja wakiwa na mwano wa kupagazwa, Uhuru. Hapa ndipo tunaelezwa vile wawili hawa walivyokutana na pia yale yaliyowatokea. Nyakti ni za usiku usiku, kuamkia sikukuu ya Uhuru. Wanasokomoko wengine, lao wanalo kushehekea kwa nyimbo na ngoma.

Mwinyihatibu mtembezi ambaye alikuwa mfanyikazi wa Mtemi alinunua shamba kule Baraka, alikoishi na familia yake akina Imani. Basi baba alipofariki, wakaja Askari na kudai kuwa

sehemu ile ya ardhi lilikuwa na mwenyewe. Kupinga walipigwa na kuachwa hali mahututi. Oscar Kambona akatorokea na kudai kuja kulipiza kisasi. Baada ya mama mtu kuzikwa, wakaja Askari na kuchoma maskani ile, nusura Imani ateketee.

Marejesho hadi mwanzo wa safari hii ya waja hawa waili. Wanapokutana kando ya ziwa

Mawewa, tunapomwona kijana mmoja, umri wa miaka isghirini hivi anaposoma hatujui nini.

Kisha anaitupa runda ile ya makaratasi baharini. Kumbe ilikuwa mswada ambao Amani kapeleka ili kuchapishwa,akarudishiwa kwa madai kwamba haikuwezekana kuchapishwa. Kumbe Amani kachezewa karata, mswada wake ukaibiwa na kuchapishwa kwa jina la Majisifu Majimarefu. Hapa basi tunashangazwa kuona kwamba ni wale wanaofaa kuwa kiegezo kwa wnagenzi, ndio wanaobadilika kuwa paka kulinda kitoweo.

Wakati ambapo walikuwa wakipiga gumzo usiku kucha, mtoto Uhuru alilala fofofo. Ndugu hawa wa kupanga, wasiojuana, wazaziye Uhuru, mtoto wa kupagazwawakavuliana siri zao. Hata Amani aliyekuwa msiri kama kaburi hakuwa na jingine ila kudondoa alicho nacho rohoni.

SURA YA TANO

Uwanja wa Nasaba Bora ambapo wananchi wansherehekea sikukuu ya Wazalendo umefumukana hadi ya kufumuka. Wameroa kwa jasho kutokana na joto jingi. Waliomo, wananchi wa kawaida hawakuchelewa kufika, saa tatu upuzi walikuwa wamefika. Acha viongozi waje wakti wao na kufika pao, walipotengewa.

Mwendo wa saa tano unusu, anafika Mtemi na aina yake. Jukwani anapanda Balozi, jamaa mcheshi na mjanja. Anayo matamu matamu yanayoweza kumtoa nyoka pangoni. Hata hivyo, anajihadhari asije akaukate “mkono uliokuwa ukimlisha au kuziuma chuchu alizozinyonya”. (uk

67)

Ingawa Balozi ni mtu aliye na ushawishi mkubwa kwa umati, hakosi kuonyesha uzembe wake kwa kumsifu Mtemi, sifa zilizo kinyume kabisa na matendo yake Mtemi Nasaba Bora. Anapowauliza wananchi ikiwa kunaye yeyote asiyempenda Mtemi, kimya kinawazidi wasiweze hata kohoa. “Anatambulikana kwa fadhili na utu wema wake…Kiongozi aliyeteuliwa na Mwenyezi Mungu.” (uk 68) Angurumapo samba, mcheza nani? Hakuna aliyethubutu ila wengine kama Mzee Matuko Weye. Hata hivyo hatukosi wale wa kunung’unika kichichini angalau wasije wakapatikana na Askari wake Mtemi, Bi Kizee akiwemo.

Wakti huu, Mashaka anapata nafasi ya kupenya na kuingia umatini anapokutana na mpenziye Ben Bella. Tunamwona Bella akimkabidhi mashaka barua na kasha Mashaka kutokomea msalani. Mvua inaanza kunyesha baada ya Mtemi kumaliza hotuba yake aliyoitoa kwa lugha ya kimombo ambapo, “kila mtu alihisi kugeuzwa…akawa bumbumbu mzungu wa reli”. (uk 70) Watu wanajaribu kujisetiri ndani ya hema aliko Mtemi na aila yake ili kuepuka mvua lakini “wanazuiliwa na Askari kwa amri ya Mtemi”. Yanapomzidi matuko Weye , anakwea jukwani na kukamata kipaza sauti. Anayabwaga yaliyo rohoni, machungu yanayomkereketa nyongo na kumshambulia Mtemi kwa ubaradhuli, unyanyasaji, dhulma na wizi. Anatunyang’anya mashamba, mali, mabinti na hata wake zetu wenyewe.” (uk 71)

DJ anamfahamisha Amani kuhusu ugonjwa wa mtoto Uhuru. Amani anajitokeza kuelekea kibandani kwake huku akicharazwa na mvua. Muda si mwingi, gari la Mtemi Nasaba linavuma

na analipisha amani, gari hili ambalo lilimpita mwanamke aliyekuwa akijifungua njiana alipotoka mkutanoni.

Amani na Imani wanaandamana kuelekea zahanati ya Nasaba Bora ili angalau motto Uhuru akapate kutibiwa. “Walipofika si mabezo hayo waliyofanyiwa na wauguzi wa kike waliokuwa wanafuma fulana zao na kupiga zohali.” (uk 76) Nashangazwa sana nay ale yanayoendelea katika vituo na maofisi za serikali tunakotarajia wananchi kuhudumiwa. Ni wangapi waliowahi kuaga dunia kutokana na vituko vya madaktari na wauguzi? Kitambo si sana, nduguye Imani kaaga, leo hii ni motto Uhuru asiye na hatia. Asiyewahi kutenda maovu yoyote.

“Maisha ni mshumaa usiokuwa na mkesho.” (uk 78) Ndivyo alivyonena amani baada ya kitoto Uhuru kulala usingizi usiokuwa na mkomo. Hata hivyo Imani hakuweza msahau kitoto kile cha kupagazwa, basi alipompata mtotowwe, basi akaamua kukiita kindakindaki Uhuru wa Pili. SURA YA SITA

Mashaka akafikishwa shuleni kwa gari la babake. Akakimbia hadi chumbani mwake na kujifungia. Akaitoa barua aliyoipata toka kwa Bella. Ndani akafahamishwa kuhusu kuvunjika kwa uhusiano wa kiushuhuba ulioko baina yao wawili; Mashaka na Ben Bella. Mtemi Nasaba Bora kampachika mimba mwana wa watu, Lowela dadake Bella. Basi Lowela kajifunga kamba

tumboni hadi wakti wa kujifungua bila ya wazaziye kufahamu. Mtemi akamtorosha na kuficha

Baraka alipopatikana na Ben na kuelezea yaliyotukia.

Wakati ambapo Ben Bella anachumbiana na Mashaka bintiye Mtemi Nasaba Bora, Mtemi naye anashuhubiana na Lowela mwanawe Bwana Maozi. Vipi ushemeji ukawezekana wakti baba na bintiye wanapendana na ndugu wawili wa damu moja? Ni uchafu na ukaidi gani tunaoupata hapa? Msomaji jiulize swali hili. Mtemi ni kiongozi mtukufu aliyechaguliwa na Mwenyezi Mungu, huku hakosi “kusuluhisha migogoro ya shamba” na kuvuna asipopalilia.

Asubuhi ya siku ya pili baada ya sikukuu ya Wazalendo, askari wakafika na kuwakabili akina Amani, waliodaiwa kumwua mtoto Uhuru, na tuhuma nyingine kuwa Imani kakosa kuhudhuria Uwanja wa Nasaba Bora kwenye sharehe.

Wakatupwa kwenye ikulu ya rais Matuko Weye, walikompata kapotea kwenye usingizi akoroma. Kelele zile za kujitetea kwa akina Amani na tani za askari zikamuamsha rais kutoka lepe lake la usingizi. “Miye mtukufu rais bado nalala na mwaniletea kelele?” (uk 85) Katika harakati za kuwakagua waziri alioletewa, wa ufisadi na magendo bora watoe kitu kidogo.

Akamwona msichana Imani. “Nenda ukaolewe weye ukazae watoto…wakaikomboe Tomoko toka kwa mkoloni mweusi.” (uk 85). Basi vituko na vitani hivi vikafikia kikomo kuliposikika ngurumo za gari la Mtemi. Kama kawaida, Yule askari mrefu akakimbia kulifungua lango la gari baada ya kupiga saluti.

Alipoketi ofisini mwake, akapokea barua na gazeti Mtemi. Akatizamatizama kwenye gazeti la Tomoko leo na kukosa picha yake. Akakumbuka kwamba kakake Majisifu alipokuwa mhariri wa gazeti lile, basi picha zake hazikukosekana ingawa kulikuwa na suintofahamu baina yao. Kufungua barua ile iliyotoka kwa mwanawe Madhubuti akafahamishwa kwamba Madhubuti angeweza kurudi nyumbani mwishoni mwa mwezi ule. Hata hivyo Madhubuti akaonya kwamba asingependa kufanya kazi zipatikanazo kwa hongo na milungura. Yeye angependa kula jasho lake mwenyewe.

Mzee Matuko alipoamriwa toka ikuluni, akadinda huku akidai, “Lakini hata mkiniua kumbukeni kwamba watazaliwa Matuku wengine watakaoendelea na harakati za ukombozi toka pale nilipoachia.” (uk 86)

Akaghadhibika sana Mtemi kutokana na barua ile. Kwa hasira na hamaki, akaamuru akina Imani kupigwa na kuteswa. “Wale mahabusu mkwafanyie kazi kama kawaida.” (uk 88) Akaliweka gari moto kuelekea janibu nyumbani kwake. Wakti huo walipokuwa wakifanyiwa kazi, Amani alibaki kunyamaza tu kama kiumbe kisichokuwa na uhai huku Imani akipiga ukwenzi uliosikika mbali.

 

SURA YA SABA

Siku tatu baada ya Mtemi kupokea barua kutoka kwa mwanawe Madhubuti, majira ya saa tatu asubuhi, kakake Mwalimu Majisifu akamtembelea kwake katika kasri la Majununi. Kukawa siku hizi, mkewe Bi Zuhura katafunwa na jakamoyo na upweke juu ya mumewe asiyesemezeka wala kuambilika. Kukawa Mtemi hawezichelewa kusuluhisha migogoro ya mashamba yake yasiyoisha.

Majisifu akapokelewa na Bi Zuhura wakawa wanapiga gumzo sebuleni. Alipotoka kukoga Mtemi, akavalia kwa muda, hajali kumsabahi. Baadaye akajitosa ukumbini aliposikia kakake kaulizia aliko. Bi Zuhura akawapa nafasi baada ya Mtemi kukaa mbali sana na wote wawili, Majisifu na Zuhura. Kimya kirefu kikajiri baina yao.

Alipojirudisha Mtemi, akamwuliza kakake majisifu kwa nini kakosekana mkutanoni. Majisifu naye akajibu kwamba kawa ameenda “ibada”. Akamwonya kakake Mtemi kuhusiana na madhara ya pombe, sana ikilinganishwa na vile baba yao kasisi kawakuza. Kujitetea majisifu akadai kwamba uovu uliofichwa ndani ya dini haumpendezi. “Afadhali nitende mambo yangu waziwazi.´(uk 93)

Mtemi akawa anampozoa Mwalimu hasira huku anajizuia kupasuka. Alipodai kujali maslahi yake Majisifu, akamwambia ajali maslahi ya Wanasokomoko wote. “Kama ungekuwa unajali maslahi yaw engine, yule mchungaji wako na mtumishi wangu hawangekuwa wanapigwa na

baridi kule ndani kwa kosa ambalo hawakulitenda.” (uk )

Chai ilipoletwa mezani, Mtemi akashangaa kuona ni ya mkandaa. Akawa hana jingine ila kuinywa ili kuficha ukweli. Ndipo akagundua ndani mna nzi mkubwa wa buluu, kakufia mle ndani. Twaona kwamba haya yote ya suintofahamu katokana na kitiwa kwa Amani mbaroni. Wakawa hawaongezani wala kusemezana. Kukawa kimya.

Yalipozidi unga, Majisifu akaaga na kutokomea mbali, ukuta wa uhasama ukakithiri baina yao. Lakini kitu kimoja walichokosa kujua ni kwamba siku hiyo kawa mwisho wa kukutana kwao katika kasri la Majununi. Hatujui kukatokea nini baadaye ila tu tusome. Kutoka kwake Mtemi bila kwaheri, Majisifu akahesabu boriti kuelekea kwa Mama N’tilie alikotarajia kuwa na ibada. Akakumbuka kwamba alikuwa na kipindi kimoja cha kufundisha lakini akadai kuwapa nafasi wale maziwa lala wakawaandikie muhibu wao barua za mapenzi na kupanga jinsi ya kukiuka vizingiti vya shule.

Hapa twajagundua kwamba Mwalimu Majisifu hakuwa na akili nzuri ya kumwezesha kuandika vitabu. “Ningekuwa na akili nzuri ya kuandika kitabu ningeandika juu ya kibe wachezacho wasichana hao na mwalimu mkuu…” (uk 98)

Akaitisha bibilia Mtemi na kuanza kusoma, kitu alichokawia kufanya miaka nenda miaka rudi. Akakumbuka kuhusu kidoshao kimoja kiguru aliabiri naye gari pamoja kuelekea mjini.

Akajitetea Nasaba lakini kakosolewa kwamba hangeweza kucheza ngoma ile hata kama ni yeye aliyeianzisha. Kutia nanga mjini, Nasaba akamwona Yule mrembo akiinama na kutoa

mikongojo miwili ya kwapani. Akagundua ukweli, upendo ukamtoka, akaomba radhi na kutokomea.

Na katika harakati hizi ndipo kukasikika ukwenzi mkali kutoka nje. Alipotazama Zuhura ili kutendua kilichosadiki, akamwona DJ yu chini huku mguu wake uking’atwa na mbwa Jimmy. Zuhura akamcharaza Yule mbwa na akatoroka asionekane tena. Akampokeza barua ile Bi Zuhura na kuomba kuondoka ili kupeleka ng’ombe wa mwajiri wake malishoni.

Basi mkewe Mtemi akamfikishia barua yake, hapo ndipo pakatokea mzozano baina yao Zuhura alipomwonya Mtemi kwa kutowachanja mbwa wake wakti akiwahukumu wale waliokosa kuwachanja wao. Kwa madharau akadai kwamba DJ alistahili alichokipata.

Kufungua barua ile, akakutana na yalimshangaza. Lowela akaonya kutoboa siri Mtemi akosapo kuwaachilia huru Amani na Imani. Ndiyo mapenzi ya masharti yake binti wa watu. “Moyo ulimpapa na kijasho chembamba juu ya mwanzi wa pua. Akahisi uchungu wa mwiba wa kujidunga.” (uk 106) Atahadhari huku maji yashammwagikia? Nani atakayeyazoa?

SURA YA NANE

Ikuluni kwa Matuko Weye kaja askari mmoja na redio aliyoitazamia kusikiliza matangazo ya mpira baina ya timu za Songoa FC na Meza Wembe kutoka Wangwani. Wakawa wote, askari na waziri, Amani na Imani wanayasikiliza matangazo hayo kwa njia mwafaka kabisa.

Mpira karibu kumalizika, Songoa ikabahatika bao moja kutoka kwa mchezaji mmoja maarufu kwa jina la Chwechwe Makweche almaarufu “Horsepower”. Imani akajikuta katikati ya fahamu, hajui amshangilie kakake kwa kuifunia Tomoko ama ahuzunike kwa kakake kuwasahau kabisa. Kidogo kukasikika mngurumo wa gari. Mtemi Nasaba kafika na kuwaamuru askari, “Wafungulieni hawa washenzi watoke.” (uk 109). Wakawa huru Amani na Imani. Lakini tujiulize, kwa nini wakaachwa huru bila kushtakiwa? Ndio wanyonge hupitia, wasio na lao, hawana mbele wala nyuma.

Kuondoka kwake Majisifu kuelekea Wangwani kulisadifiana na kurudi kwake Madhubuti kutoka Urusi. Huku Amani na Imani wamesharudi kazini, Amani akatunga beti kuhusu mwanawe wa kupanga, Uhuru. Baadaye akajaribu kutunga nyingine kwa heshima ya rafikiye DJ, akashindwa, kwani maneno hayakuitwa yakaitika. Twaona kwamba DJ kafikishwa zahanati ya Nasaba Bora baada ya hali yake kuwa mbaya, huku adinda kunengua kilichokuwa kimemsadiki.

Miaka mingi baadaye Imani kamsihi Amani iiandike tawasifu kuhusu maisha yake, hakukosa kudukia yaliyomo baina yake na Madhubuti. Walikuwa masahibu wa chanda na pete, hata wengi walishangazwa alipohamia Madhubuti kibandani mwake Amani.

Wakawa wamepatana. Madhubuti akiwa tayari kwa mapinduzi naye Amani akiwa tayari kupiga jeki. Mtemi haelewi yaliyomkuta mwanawe. Madhubuti alipoajiriwa Songoa, wakawa wanawasiliana kupitia nyaraka. Madhubuti akawa marafiki na maofisa wa wizara ya ardhi kwa lengo la kupasua mbarika alikotokea Mtemi kumiliki mashamba mengi na makubwa makubwa kama vile.

Tangu Mashaka kupata barua toka kwa Ben Bella, akawa “mnuni,kama kondoo” (uk 121). Aliathiriwa sana na yale yawapatayo waliowachana kimapenzi. Akakatiza masomo na kurudi nyumbani. Juhudi za wazaziye kumsihi akarudi skulini zikaambulia patupu, mtoto akawa kisiki hasikii.

Majisifu naye akafika chuo kikuu cha Mkokotoni kulikojaa sisisi, macho kama elfu za na zaidi. Akakaribishwa na kasha kupewa nafasi akahutubu. “…alikumbwa na kiherehere na kohoro.” (uk ) Ahaa! Mambo yanamwendea zegemnege. Akafungua mkoba wake huku kijasho chembamba kinamtoka. Akaangusha karatasi zake kutokana na uoga na kiwewe. Akarudi na kuketi chini

huku umati ukiangua kicheko.

Baada ya mhadhiri mmoja kunong’onezana naye kwa muda, ikasemekana kwamba hangeweza kuhutubu moja kwa moja, basi ikabidi wahadhiri waulize maswali huku Majisifu akiyajibu. Akaulizwa kwa nini akachagua anwani “Kidagaa Kimemwozea” kwenye kitabu chake. “Kwa kweli sijui ee, sijui kwa nini nilchagua kukiita kitabu hicho, Kidagaa Kimemwozea. Niligutuka tu nimekiita hivyo.” (uk 123)

La pili akaulizwa maoni yake kuhusu jinsi mataifa ya Afrika baaada ya mkoloni. “Kuna umoja na utangamano humu barani. Viongozi wa Afrika huru wameshika usukani kwa njia bora zaidi. Afrika imekombolewa toka kwa matatizo ya njaa, umaskini na ujinga.” (uk 123-124)

Akajikuta hawezi kujibu maswali kwani majibu yake yalitfautiana sana na maoni yake kwenye “Kidagaa Kimemwozea”. Akajitetea, “La! Mimi sikuonyesha hivyo kamwe katika riwaya hiyo.” (uk ). Basi nani kaonyesha, na hata hivyo, yanaonekana hata Mwalimu Majisifu hakuwa amekisoma kitabu hicho.

Wahadhiri wakashangazwa hadi ya kushangazwa. Swali akalipata kuhusu hali ya Kiswahili. Akajibu, “Kiswahili kitaendelea kuimarika vyema lakini sharti tuondoe Watanzania na Wakenya kwenye ulingo…Watanzania wanadhania kwamba ni wao tu ndio wakijua Kiswahili na Wakenya wanafikiria kwamba kulipua makombora ya misamiati…” (uk 125) Kukalipuka kicheko. Akaulizwa ikiwa kaandika riwaya ya “Kidagaa Kimemwozea” na kwamba kulikuwa na fununu kuwa kauchukua mswada wa mtu mwingine. “hayo yalikuwa mno.” (uk 125) Akafyata ulimi, huku unga umemzidi maji. Hata hivyo akaokolewa na mhadhiri mmoja aliyedai kuwa hotuba ingeendelea siku iliyofuatia.

Jioni hiyo, Majisifu akaabiri ndege kurudi Tomoko huku yu tayari kulipa fidia ikibidi. Akajikuta “atokwa na machozi kama mtoto mdogo.” (uk 127) Akajuta Majisifu, kumbe kidagaa kilikuwa kimemwozea.

 

SURA YA TISA

Alidhania hawezi kufa hata alipowadhalimu na kuwatesa wananchi wasio na hatia. Akaanza kupanga mazishi yake huku ajihisi marehemu. Siku moja kamwita Amani na kumpa sururu, jembe na sepetu. “nataka uchimbe hapa kaburi langu. Siku nitakapokufa nataka kuzikwa hapa.” (uk 128) Ingawa Amani hakulitegemea, akawa hana budi ila kukamilisha jukumu lake. Hivyo basi, akalichimba kaburi hilo kwa siku tatu, likawa la fahari.

Mashaka kwake kukawa mashaka kweli, habebeki mwana wa watu. “Abwajabwaja ovyoovyo kama Mzee matuko Weye. (uk 129) Masomo keshaikatiza, nguo katupa na kuzura tupu mitaani. “Kumbe chema hakidumu.” (uk 129) Madhubuti amejitolea kutumikia nchi yake kwa moyo wake wote, tendo lililokuwa mkabala na alivyoamini baba mtu. “…alielewa fika kwamba ingebidi aukate mkono uliokuwa ukimlisha tangu hapo hata matokeo yake yakiwa nini.” (uk 130) Mashaka akaleta rabsha na kuwazidi wafanyikazi wengine. Bi Zuhura akamwita Amani na pamoja wakamfungia Mashaka chumbani mwake. Kwa kuogofya yaliyokuwa yakiendelea, Bi

Zuhura akamsihi Amani kalale ukumbini. Nyakti za usiku, Amani akaitwa na Bi Zuhura ili kaangalie ni nini kilichokuwa chini ya kitanda chake mama mtu. Ni katika harakati hizi ndipo Bwana Mtemi akarejea na kuwakuta wawili chumbani, wanatetemeka. “Ndani kukawa hakukaliki, nje hakutokeki.” (uk 131) “Kumbe huyu mwanamke huniendea kinyume na mfanyikazi jamani?” (uk 131) Akafungua sefu Mtemi, akatoa bunduki na kumshambulia. Alipodiriki kwamba Amani kaaga dunia, akambeba kwenye buti ya gari lake na kumtupa kando yam to Kiberenge, ambako aliokotwa na Wasamaria wema na kupelekwa zahanati ya Nasaba Bora.

Kukawa siku nyingi zimepita Amani akiwa zahanatini. Alipofumbua macho na kisha kuachwa huru, Imani wakaambatana na Majisifu kumpeleka kwake Majisifu mwenyewe. Amani kufika nyumbani, akakubaliwa kukaa katika “servants quarters” huku bado hawezi kuongea na kuwasiliana kwa kuandika. Imani akamchunga kakake vizuri sana.

Amani akamfahamisha Imani ya kuwa angependa kujistarehesha kwa kusoma vitabu. Imani akamwazimia vitabu kutoka kwa Mwalimu Majisifu, ikiwemo kimoja kwa anwani la “Kidagaa kimemwozea”. Kwa mshangao, kitabu chenye picha ndicho kile chake, mswada aliyorudishiwa kwa kuwa hauwezi chapika. Majisifu kajikuta taabani. “Lililomshangaza ni kwamba Yule aliyeitwa mwandishi na kupachikwa picha yake katika jalada la nyuma, hakuwa ndiye mwandishi wa kitabu hicho.” (uk 140) “…kilichokuwa chake kimekuwa cha mwingine.” (uk 141) Amani akamwandikia Imani barua kumwelezea juu ya le aliyoyaona. Majisifu akaipata barua ile na kuisoma. Hapo Imani akampata na kumkabili vipasavyo. Majisifu akatoa zote siri alizokuwa

amezibana, “Kumbe umdhaniye ndiye siye?” Akamwandikia karatasi ndogo Amani kwa Majisifu.

 

MASWALI

1. Je kuna umuhimu gani wa hadithi ndani ya hadithi kama ilivyotumika katika riwaya ya

“Kidagaa Kimemwozea”?

2. Eleza jinsi riwaya ya Kidagaa Kimemwozea ilivyoakizi jamii halisi ya Kenya ya sasa.

3. Eleza matatizo yanayowakumba vijana kwenye riwaya ya Kidagaa kimemzea.

4. Thibitisha maudui ya ufisadi katika riwaya ya Kidagaa Kimemwozea.

5. Eleza jinsi maudhui yaq uteleleshi imejitokeza katika riwaya ya Kidagaa kimemwozea.

6. Eleza athari za ukoloni mamboleo.

7. Kidagaa kimemwozea ni anwani inayodokeza kuharibikiwa kwa mambo. Jadili ukweli wa kauli huu.

8. Ukengeushi ni mojawapo ya matatizo yanayozikumba jamii za Afrika. Thibitisha kwa kurejelea riwaya ya Kidagaa Kimemwozea.

9. Eleza jinsi mbinu ya majazi imetumika katika riwaya ya Kidagaa kimemwozea.

10. Mbinu ya kinaya imetumika vipi katika riwaya ya Kidagaa Kimemwozea. Thibitisha.

11. Pana mbinu ya ishara katika riwaya ya Kidagaa Kimemwozea. Itambue ishara hiyo na kueleza inachoashiria.

12. Taja na ufafanue mifano miwili ya methali iliyotumiwa katika riwaya ya Kidagaa

Kimemwozea.

13. Taja sifa mbili za Mtemi Mtemi Nasaba bora ukirejelea riwaya ya Kidagaa Kimemwozea.

14. Eleza jinsi mbinu ya taharukiimejitokeza katika riwaya ya Kidagaa Kimemwozea.

15. Anwani ya Kidagaa Kimemwozea ingeweza kuitwa Songoa. Jadili kwa kutoa mifano mwafaka.

16. Mbinu ya utabiri imetumikajae katika riwaya hii iliyosukwa ikasukika?

17. Eleza jinsi kiangaza mbele ilivyotumika katika riwaya hii.

18. Uwendawazimu wa Weye si uwendawazimu tu! Bali kuna ukweli na uhakika fulani ndani yake. Jadili.

19. Taja na ufafanue wahusika waliozewa na kidagaa.

20. Eleza sababu ya Amani kutupa mswada ziwani.

21. Amani na Madhubuti wanaleta mwamko mpya katika eneo la Sokomoko. Thibitisha.

22. Jazanda imejitokeza vipi katika riwaya hii?

23. Kidagaa ni nini na kimemwozea nani?

b) Toa sababu ya kidagaa kuoza.

24. “Mgalla muue na haki umpe.”

a) Eleza muktadha wa dondo hili.

25. “Hakuna refu lisilokuwa na ncha.”

a) Elezea ufaafu wa methali hii ukirejelea maisha ya Mtemi Nasaba Bora.

26. “Sijawahi ona kibogoyo akiguguna mifupa, waweza andika nini wewe?”

a) Lihakiki dondoo hili.

27. “Nimekuwa ganda la mua”.

a) Eleza muktadha wa dondo hili.

b) Anayelengwa na maneno haya amekua ganda la mua. Fafanua. c) Jadili kuharibikiwa kwa wahusika hawa.

28. “Penye nia pana njia tena usione wembamba wa reli gari moshi hupita na mdharau biu hubiuka”. Eleza muktadha wa dondo hili.

29. “Tukisema hatuna viatu tunaambiwa wapo watu hawana miguu.”

a) Eleza muktadha wa dondoo hii. b) Taja sifa za msemaji.

c) Eleza umuhimu wake katika riwaya ya kidagaa Kimemwozea.

30. “Pengine imeandikwa kwamba tusioane. Narudi kwetu. Katafute mwanamke kufu yako.”

a) Eleza muktadha wa dondoo hili.

31. Taja na ujadili wanandua walioharibikiwa ndoa kwa mujibu wa riwaya hii.

32. “Álikuwa mtoto wa mjane aliyepika pombe haramu mtaa wa Madongoporomoka.”

33. Taja na ueleze sifa za mhusika anayerejelewa.

34. “Mwandishi kama huyo watu hukutana naye kwa nadra sana.”

a) Eleza muktadha wa dondoo hili.

35. Jadili umuhimu wa mhusika huyu katika riewaya ya kKidagaa kimemwozea.

36. “Nimekuambia hutaweza kuisakata ngoma hii hata ndiwe uliyeianzisha mwenyewe.”

37. Eleza muktadha wa dondoo hili.

38. “Kweli kidagaa kimemwozea Mtemi Nasaba Bora.”

39. Thibitisha ukweli wa kauli hii ukirejelea mifano katika riwaya ya Kidagaa Kimemwozea.

40. “Nyani haaoni kundule.” Ukitumia hadithi hii, jadili maudhui ya mapenzi ukirejelea riwaya ya Kidagaa Kimememwozea.

41. “…wakati alipokuwa akiandika tawasifu wake miaka mingi baadaye…”

a) Liweke dondoo hili kwenye muktadha wake. b) Taja mbinu ya lugha iliyotumiwa hapa.

c) Eleza sifa zozote tatu za msemwa wa maneno haya.

42. “Kwa nini kimeletwa na kuwekwa mlangoni pangu?”

a) Eleza muktadha wa dondoo hili. b) Taja mbinu za lugha zilizotumika.

c) Ni maudhui gani yanayochipuka kulingana na dondoo hili?

43. “Hawapikiki chungu kimoja kama mbuzi na chui.”

a) Eleza muktadha wa dondoo hili.

b) Taja na ufafanue sifa mbili za wahusika warejelewao.

44. “Alikuwa mumunye aharibikiaye ukubwani.”

a) Andika wasifu wa mhusika anayerejelewa.

45. “Akijikuna hutoka unga.”

a) Taja na ufafanue mbinu ya uandishi uliotumika.

b) Je, ni sifa zipi tano zinazomilikiwa na mhusika aliyerejelewa?

46. “moyo ulimrindima kwa rindimo la kumbwaya na la msondo.”

a) Liweke dondoo hili kwenye muktadha wake.

b) Taja mbinu za lugha zilizotumika.

47. Hapa ndipo Fao kajigeuza paka kulinda kitoweo.”

a) Taja wahusika wengine wawili walio na sifa kama za mhusika anayerelewa. b) Jadili maudhui yanayojitokeza katika dondoo hili.

48. “Alitunga na kutungua huku makisio na magozo ya kila aina yakimpitikia kichwani.”

a) Je ni nini umuhimu wa mhusika anayerelewa katika riwaya ya Kidagaa Kimemwozea?

49. “Mume mwenyewe huyu kwa kweli habebeki kama mzigo wa moto.”

a) Ni mhusika yupi anayeyatamka maneno maneno haya na anamlenga nani?

b) Ni mbinu gani ya uandishi unaojitokeza?

50. “Yatima hajizuruku mwenyewe.”

a) Swala la uyatima ni moja kati ya maudhui yanayoangaziwa kwa kina katika riwaya ya

Kidagaa Kimemwozea.

i. Taja wahusika wane mayatima katika riwaya hii.

ii. Ni changamoto zipi mayatima hukumbana nazo katika jamii?

51. “Akakohoa kohozi kavu na kupiga usiahi mkali kama king’ora cha polisi wakati wa dharuara.”

a) Liweke dondoo hili katika muktadha wake.

b) Eleza yaliyokuwa yamejiri kabla ya mabo haya yanayotendeka kwa sasa.

c) Ukirejelea mhusika huyu, taja na ueleze maudhui yanayojitokeza kulingana na riwaya ya Kidagaa Kimemwozea.

52. “Kuondoka kwa Mzungu kulileta kheri na ghanina.”

a) Jadili faida walizozipata Waafrika toka kwa mkoloni barani Afrika.

b) Jadili madhara yaliyowakumba Waafrika kutokana na kuwepo kwa mkoloni barani

Afrika.

53. “Alitahadhari sana asiukate mkono uliokuwa ukimlisha au kuziuma chuchu alizozinyonya.”

a) Eleza muktadha wa dondoo hili.

b) Ni maovu gani huendelezwa na viongozi ukizingatia alivyoshawiriwa mhusika huyu?

54. Ngoja ngoja haiumizi matumbo, inaupa moyo subira.”

a) Je, unakubaliana na kauli ya maneno haya? Jadili

b) Ni mambo gani yaliyokuwa yametendeka yaliyomfnya mhusika kusema maneno haya?

55. “Kichwa cha kuku hakihistamili kilemba.”

a) i) Ni mhusika aliyevishwa kilemba asichokihistahili?

ii) Ni mambo gani aliyoyatenda yaliyomfanya avishwe kilemba?

b) Jadili kauli ya msemo huu ukirejelea riwaya ya Kidagaa Kimemwozea.

56. “Ukikosa la mama hta la mbwa huamwa.”

a) Taja sifa za mhuski anayerelewa.

b) Mhusika huyu ni mmoja kati ya wale waiowahi kuhukuwa vifungo kwa kusinziwa makosa.

i. Ni makosa gani haya aliyosinziwa?

ii. Taja wahusika wengine watatu waliohukumiwa bila haki kutendwa. c) Jadili maovu ambayo mahakama huwatendelea wanyonge.

57. “Kulea mimba si kazi, kazi ni kulea mwana.”

Swala la uwajibikaji ni moja kati ya maudhui yaliyoangaziwa katika riwaya ya Kidagaa

Kimemwozea.

a) Kuna wazazi wawili wanaojitokeza kutojali haki za watoto na kumtupa mtoto wao kwenye bardi kali la machweo huku yu uchi.

i. Je, ni matendo yepi yasiyo ya kawaida au ya nidhamu yanayotendwa na wazazi hawa? ii. Je, ni madhara yepi yanayowakumba wahusika wengine kutokana na matendo ya wazazi hawa?

b) Kwa kifupi, elezea wasifu wa mhusika aliyetupwa gizani alfajiri.

58. “Alijiona maskini wa mapenzi.”

a) Kati ya maudhui yaliyoangaziwa katika riwaya ya Kidagaa ni pamoja na swala la mapenzi na ndoa.

i. Taja visa sita vya mapenzi baina ya wahusika katika riwaya ya Kidagaa Kimemwozea. ii. Jadili madhara yanayotokana na uhusiano wa kimapenzi baina ya vijana wadogo katika jamii.

59. “Ndugu wawili wakigombana shika jembe ukalime, wakipatana chukua kikapu ukavune.”

a) Je, kauli hii inarejelea wahusika wepi katika riwaya hii?

b) Ni mambo gani yaliyotokea maishani mwa wahusika yaliyowafanya kugombana?

c) Linganisha kauli hii na msemo “damu nzito kuliko maji”.

60. “Achekaye kilema hafi hakijamfika.”

a) Jadili kauli hii ukirejelea riwaya ya Kidagaa kimemwozea huku ukizingatia funzo kwa jamii.

b) Fafanua baadhi ya matatizo yalimpata mhusika huyu aliwacheka vilema katika riwaya hii.

61. “Akahisi uchungu wa mwiba wa kujidunga.”

a) Liweke dondoo hili katika muktadha wake.

b) Taja na ufafanue umuhimu wa mbinu ya lugha iliyotumika katika dondoo hili. c) Taja wahusika wawili waliohisi uchungu wa mwiba wa kujidunga.

62. Eleza mbinu ya majazi kama ilivyojitokeza katika riwaya.

63. Linganisha wasifu wawahusika wafuatao na uonyeshe umuhimu wao katika riwaya ya

Kidagaa Kimemwozea.

a) Mtemi Nasaba Bora b) Amani

64. Jadili madhara yanayotokana na kuvunjika au kuharibika kwa ndoa kwa kurejelea riwaya ya Kidagaa kimemwozea.

65. Onyesha jinsi shairi la utangulizi linaoana na riwaya ya Kidagaa kimemwozea.

66. Mtemi Nasaba Bora ni miongoni mwa wanaochochea uhuru wa Tomoko. Thibitisha.

67. Toa sababu ukizingatia maudhui kwa nini watu walisusia matumizi ya maji ya mato

Kiberenge.

68. Toa sababu za Amani na Imani kufunga safari kuelekea Sokomoko.

69. Umaskini umejitokeza vipi katika riwaya ya Kidagaa Kimemwozea?

70. Swala ambalo linalojitokeza waziwazi katika kitabu hiki ni kwamba viongozi wanaendeleza zile sera mbovu za wakoloni kuongoza Wanasokomoko.

a) Thibitisha.

b) Taja mbinu ambazo za viongozi hutumia kuendeleza uongozi mbaya.

71. Uongozi mbaya huchangiwa na wananchi wenyewe. Jadili ukirejelea riwaya ya Kidagaa

Kimemwozea.

72. Chanagamoto zinazokabili ukuaji wa lugha ya Kiswahili kulingana na Mwalimu Majisifu ni yepi. Jadili ukizingatia manufaa ya lugha hii kwa jamii ya Afrika Mashariki.

73. Hakiki mfumo wa elimu katika nchi ya Tomoko.

74. Thibitisha maudhui ya ukatili katika riwaya ya Kidagaa Kimemwozea.

75. Eleza namna ya uongozi mbaya unavyoendelezwa katika riwaya ya Kidagaa

Kimemwozea.

76. Riwaya ya Kidagaa Kimemwozea inaibua maswala ya elimu na uwajibikaji. Hakiki kauli hii.

77. Fahali mmoja mweusi anaizoa suruali moja kuukuu linalomilikiwa na kijana mmoja mneni sana.

a) Ukizingatia umuhimu wa fahali hili mweusi, ni madhara gani mwandishi angeweza kukumbana nazo fahali hili lingekosekana?

b) Tendo la fahali hili linaashiria funzo gani kwa jamii ukirejelea riwaya ya Kidagaa

Kimemwozea?

78. Kando na utangamano baina ya wahusika kadhaa katika riwaya ya Kidagaa

Komemwozea,kuna utengano baina ya wahusika na tabia Fulani katika jamii.

a) Na kufafanua baadhi ya mambo yanayosababisha wahusika kutengana na wenzao au na tabia Fulani maishani.

b) Elezea faida wanazozipata wanajamii kutokana na kutengana kwa wahusika hawa na vitendo Fulani maishani.

79. Kupitia mto Kiberenge, mwandishi anapata nafasi nyingine ya kuendeleza masimulizi yake.

a) Eleza sababu zinazowafanyaWanasokomoko kususia maji yam to kiberenge.

b) Kutumia maji yam to Kiberenge ni mwiko kwa wanajamii ya Sokomoko, je imani zipi walizo nazo wahusika wanauvunja mwiko huu?

80. Kasri la Majununi, ufujaji wa mifugo na upanzi wa mimea yaletayo faida ni baadhi ya mambo yanaridhiwa na waafrika toka Wazungu.

a) Jadili mambo mengine yanayoridhiwa na Waafrika kwa mkoloni mweupe.

b) Jadili baadhi ya maovu wanayokumbana nayo Waafrika wanyonge kutokana na dhulma za viongozi madikteta.

81. Mfumo wa elimu ni kati ya sera za mkoloni unaoigwa na Waafrika. a) Taja baadhi ya wahusika wanaofaidika na mfumo huu wa elimu.

b) Katika ulimwengu mamboleo, viongozi wengi huchaguliwa katika Nyanja tofautitofauti si kwa kulingana na tajriba zao bali kwa viwango vyao vya elimu. Basi viongozi hawa wanapoingia katika afisi za serikali, wao huhusika katika na mambo Fulani ya utovu wa nidhamu kwa mfano:

i. Kuhusiana kimapenzi na wanafunzi na hata kuwatunga mimba.

ii. Kuficha faili ili wanaotafuta huduma kutoa hongo kabla ya kuhudumiwa.

iii. Kuiba mawazo na fikra za wale wanaofaa kuwaelekeza kwa mfano miswada n.k..

iv. Kuiba hela za usaidizi zinazofaa kutumiwa kuwaelimisha watoto maskini na hata za kujenga hospitali.

v. Kuhonga maofisa serikalini, k.m mahakamani ili kubatilisha uamuzi na kuwahukumu wanyonge.

vi. Kutumia nguvu kuwanyanyasa, kuwaua na kuwanyang’anya wanyonge mali yao n.k. Je, ili kuwe na mabadiliko yatakayowafanya wananchi wote kupata haki zao za kimsingi na kuweza kuendeleza maisha yao kwa amani na njia adilifu bila kusumbuliwa na sera mbovu za viongozi, jukumu au hatua zipi zinazofaa kuchukuliwa na wananchi?

82. Amani anakataa ombi la wananchi ya kuwa mtemi baada ya kufariki kwa Mtemi Nasaba

Bora. Je, kulingana na maoni yako, unafikiri hatua aliyoichukua Amani ni wa wosia? Jadili.

83. Wakati Mwalimu Majisifu alipokuwa akitoa mhadhara katika Chuo Kikuu cha Mkokotoni, akaulizwa maoni yake kuhusu jinsi ya mataifa ya Afrika baada ya Mkoloni. a) Jadili maoni aliyoyatoa kuhusu swala hili.

b) Je, kulingana na jawabu lake, “La! Mimi sikuonyesha hivyo kamwe katika riwaya hiyo”, unakubaliana na mimi kwamba Majisifu hakukuwa amekisoma kitabu hicho cha Kidagaa Kimemwozea? Jadili.

84. Mara nyingi ndoa nyingi huvurugika kutokana na uhusiano baina ya wafanyakazi na waajiri wao kote ulimwenguni kama vile tuonavyo baina ya Bi Zuhura , Nasaba Bora anapowafumania Amani na Bi Zuhura chumbani.

a) Jadili harakati na jinsi ya mipaka ya uhusiano unaofaa kuwa baina ya watumishi na waajiri wao ili kuepukana na matatizo kama tuonavyo katika riwaya ya Kidagaa kimemwozea?

b) Fafanua baadhi ya ya mambo yanayopelekea wajiri kuingiliana kimapenzi na watumishi wao.

85. Kulingana na riwaya ya Kidagaa Kimemwozea, vyombo vya dola wanatumiwa na viongozi wao kuwanyanyasa na kuwatesa wananchi badala ya kuwalinda na kuwatunza, kitendo kilicho mkabala na linalofaa kuwa jukumu la polisi na walinda usalama.

a) Kwa maoni yako, ni hatua gani zinazofaa kuchukuliwa ili kuwe na uhusiano mwema baina ya

polisi na wananchi?

b) Polisi wamekuwa katika mstari wa mbele kuendeleza hongo na milungura. Ni hatua gani inayofaa kuchukuliwa ili kuwe na Afrika huru isiyoendeleza hongo?

86. Kuishi pamoja kwa Amani na Imani kwa muda mrefu bila bila kupita mpaka uhusiano wao kimwili ni funzo kuu kwa vijana ambao huangukia mitego ya anasa. Tendo hili kati ya vijana hawa wawili ni moja kati ya njia za kuepukana na zimwi la UKIMWI, magonjwa ya zinaa na mimba zisizopangwa.

a) Ukilinganisha na matatizo wapatazo walemavu, jadili madhara ya ugonjwa wa UKIMWI

katika jamii.

87. Tukirejelea riwaya ya Kidagaa Kimemwozea, tunakutana na wahusika kadhaa walio na uraibu wa kutumia madawa za kulevya.

a) Taja na kutoa sifa mbili za wahusika wawili walio na uraibu huu.

b) Jadili madhara zitokanazo na matumizi ya madawa ya kulevya katika jamii.

88. Mtemi Nasaba Bora anatoa hotuba ya Rais kwa lugha ya mkoloni isiyoeleweka na wengi wa wananchi. Kati ya wale wasiopendezwa na hotuba hii ni Bi Kizee anayenung’unika kichinichini.

a) Taja wahusika wanne waliojitoa hadharani kupinga mfumo huu mbaya wa uongozi.

b) Jadili baadhi ya mambo wayatendao wananchi yanayosaidia viongozi wadhalimu kuendeleza sera zao za kikatili.

89. Si jambo la kawaida kila mtu anapozaa kujifungua vilema. Bwana Majisifu anamlaumu

Bi Dora kwa kumzalia mashata.

a) Ni sababu zipi anazozitoa Majisifu ili kujikinga na na ukweli kwamba lazima kachangia katika kuwazaa wale watoto walemavu?

b) Kulingana na wataalamu wa kiafya, madawa ya kulevya pamoja na matumizi ya pombe huweza kuchangia ulemavu kwa watoto ambao bado hawajazaliwa. Hakiki kauli hii.

90. Methali “atafutaye hachoki, akichoka keshapata” inaweza kutumiwa kueleza juhudi na uwajibikaji kama ilivyosawiriwa katika riwaya ya kidagaa Kimemwozea.

a) Ukirejelea mhusika mmoja katika riwaya hii, hakiki kauli ya methali hii.

b) Je unakubaliana na mimi kwamba hatua alizozichukua mhusika huyu zilikuwa thabiti?

91. “Lakini…hakujikaza tu kisabuni, alikuwa na imani na ndiye aliyekuwa wa kwanza kuwatendea watoto haokama wanadamu.

a) Ni mhusika yupi anayerejelewa?

b) Mhusika huyu karibu ajikatishie maisha yake, hata hivyo, baadaye anajitokeza kuwa mmoja kati ya wakombozi wa Tomoko iliyokuwa Uhuru wa pili.

i. Je ni sababu zipi zilizomfanya kutaka kujiua?

ii. Unakubaliana na mimi kwamba hatua aliyiochukua kutaka kujiua haikuwa ya wosia?

92. Kati ya tunu za taifa ni pamoja na:

a) Utu

b) Uwajibikaji c) Uzalendo d) Uadilifu

e) Umoja f) Uwezo

g) Lugha ya Taifa.

Elezea maana ya huzu hizi huku ukidokoa umuhimu wao kwa jamii.

93. Elimu ni kati ya mahitaji halisi kwa kila mwananchi duniani kote.

a) Ukitoa mifano nyingine ya mahitaji halisi, elezea umuhimu wao katika ujenzi wa taifa.

94. Madawa ya kulevya yamekuwa miongo mwa vitu vinavyochochea ukosefu wa amani na maendeleo ya jamii.

a) Kwa kutoa mifano, elezea madhara ya madawa ya kulevya kwa jamii nzima.

95. Lugha ya taifa husaidia kwa kuleta utangamano baina ya jamii mbalimbali kama ishara

ya umoja na udugu.

a) Elezea faida nyingine ambazo hupatikana kwa kukuza lugha hii.

96. Vta vingi vilivyopiganiwa ulimwenguni vimechangiwa na swala la umiliki wa ardhi na rasimali.

a) Jadili namna malumbano haya yanaweza kusuluhishwa ili kuwe na amani ulimwenguni.

97. Tofauti za uongozi uliosheheniwa na ukabila na utowakilishaji sawa kijinsia ni kati ya mambo yaliyochangia kuvurugika kwa amani katika jamii.

a) Ni hatua gani zitakanazo kuchukuliwa ili kuwe na umiliki sawa ya rasimali na mengine muhimu?

98. Kulingana na Prof. Ken walibora katika kitabu chake, “Kidagaa Kimemwozea”, maovu mengi hufichwa katika dini na vita vingi kupiganiwa kwa jina la Mungu.

a) Huku ukitoa mifano ya vita ulimweguni, hakiki kauli hii.

99. Kuna waandishi wengi waliobobea katika lugha ya Kiswahili nchini Kenya na Tanzania. Ila kulingana na riwaya ya Kidagaa Kimemwozea, waandishi si halali bali matapeli wa ubunifu wa wengine.

a) Ili kumaliza utapeli huu wa wizi wa mawazo, ni hatua zipi zafaa kuchukuliwa ili kuzuia njama kama hizi.

100. Huku ukirejelea mawazo ya waandishi wengine katika vitabu ulivyovisoma, linganisha fikra zao kuhusu hali ya mataifa ya Afrika baada ya ukoloni.




Share this:


subscriber

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Accept Our Privacy Terms.*