Share this:

Maswali ya Insha za kiuamilifu

1.  Andika mahojiano baina ya mkuu wa wilaya na mwandishi wa habari kuhusu utovu wa usalama wilayani mwako.  

 

2.  Hali ya usalama imekuwa ikizorota katika lokesheni yako. Andika barua kwa chifu wa

eneo lenu ukionyesha visa vya ukosefu wa usalama na upendekeze njia za kukabiliana na

hali hiyo.

 

3.  Umealikwa katika ofisi ya mkuu wa wilaya kupendekeza njia za kukomesha uadui

unaotokana na ukabila nchini. Andika mazungumzo jinsi yalivyoendelea.

 

4.  Wewe ni kiranja anaye husika na masomo shuleni mwako. Mwandikie kiranja anayehusika

na masomo katika shule jirani ukiwaalika wanafunzi wake katika mjadala shuleni mwako.

 Ambatanisha ratiba itakayofuata siku hiyo.

 

5.  Kitengo kinachohusika na usalama barabarani kimekuchagua wewe kama mwanajopo kati ya

wanachama watano. Mmetakiwa kuchunguza kinachosababisha ajali nyingi nchini na kutoa mapendekezo yenu jinsi ya kurekebisha hali hiyo. Andaa ripoti yenu.  

ecolebooks.com

 

6.  Umehudhuria mkutano wa vijana kujadili njia za kuboresha maisha ya vijana katika jamii.

 Andika kumbukumbu za mkutano huo.  

 

7.   Umefikishwa hospitalini ukiugua. Andika mahojiano kati yako na daktari

 

8.   Wewe ni Afisa Mkuu wa Polisi wilayani mwenu; Andika kumbukumbu za mkutano wa kamati

ya usalama uliofanyika hivi karibuni kuhusu mikakati ya kuimarisha usalama wilayani humo.

 

9   Suala la ufisadi limekuwa tatizo sugu katika jamii ya Kenya. Andika mahojiano kati ya

mwenyekiti pamoja na Afisa wa Sheria katika Tume ya Kupambana na Ufisadi nchini

na mwandishi wa habari juu ya mbinu za kupambana na ufisadi.  

 

10.  Mkuu wa mkoa wa Tuinuane ameongoza mkutano wa viongozi mkoani uliojadili kuhusu

  amani na maridhiano baada ya vita vya kikabila mkoani humo. Andika kumbukumbu za  

mkutano huo

 

11.  Matokeo ya mtihani wa kitaifa wa kidato cha nne yametangazwa. Imesadifu kwamba wewe

ndiye mwanafunzi bora katika Mkoa wa Magharibi. Mwanahabari wa Gazeti la

Tujivune amekutembelea nyumbani kwenu. Andika mahojiano yenu.

 

12.  Wewe ni Katibu wa kamati ya chama cha wazazi na walimu shuleni mwenu. Andika kumbukumbu za mkutano uliofanyika hivi karibuni.

 

13.  Kumetokea mzozo wa kisiasa nchini mwako. Mmealika msuluhishi kutoka nchi jirani.

Andika mahojiano baina ya msuluhishi huyo na mwanasiasa.  

14.  Shule yenu ilishiriki hivi majuzi katika mashindano ya riadha ya shule za Sekondari

wilayani. Ulikuwa mmojawapo wa washiriki. Andika ripoti kuhusu mashindano hayo.  

 

15.  Mhariri wa gazeti la Jicho Pevu ametangazia wasomaji katika toleo la Jumatano kutuma makala

 yao ili kuchangia katika kuandika tahariri itakayohusu mabadiliko ya hali ya anga na athari zake

  katika toleo la Jumapili. Andika makala yako.

Majibu ya Insha za Kiuamilifu

1.   Mahojiano

(a) Mwanafunzi aendeleze mahojiano baina ya watu wawili  

(b) Yahusishwe maswali na majibu

(c) Maswali yalenge mambo muhimu katika mada

(d) Lugha iwe ya mnato, komavu na ya kuvutia

(e) Pawe na msamiati unaohusiana na mada

(f) Mhoji awe na utaratibu mwafaka wa kuuliza maswali katika utiririko

(g) Insha ichukue sura ya kitamthilia  

SURA

  • Pawe na majina /cheo/vyeo vya mhoji /mhojiwa
  • Herufi kubwa au ndogo itumiwe
  • Matumizi ya hisia au masolugha yawe mabanoni (vicheko, furaha)- iandikwe kwa kifupi

Mifano ya utovu wa uslama ni kama;

  1. Uzembe  
  2. Umaskini  
  3. Ufisadi
  4. Ukosefu wa elimu katika jamii  
  5. Kuvunjika kwa taasisi za jamii (k.m ndoa, elimu)
  6. Wizi wa kimabavu
  7. Kuvamiwa na genge lililo mafichoni
  8. Vita katika nchi jirani
  9. Watoro kusababisha michafuko katika sehemu walikohamia
  10. Silaha hatari bila idhini
  11. Ulanguzi wa madawa ya kulevya
  12. Ukosefu wa kazi

 

2.  Hii ni barua rasmi  

  Iwe na sura ifuatayo:

  1. Anwani mbili; ya mwandishi na mwandikiwa
  2. Sehemu ya maamkuzi; kwa Bw/ Bi
  3. Mtajo: KUH: YAH: (Kiini cha barua)
  4. Mwili wa barua Sehemu ya maudhui (Hoja)
  5. Hitimisho au mwisho wa barua

Mimi wako………

 Sahihi

 Jina

 Baadhi ya hoja za insha

 Visa

  • Wizi
  • Mauaji
  • Matumizi ya dawa ya kulevya
  • Unajisi/ubakaji
  • Magenge ya majambaz

 

Mapendekezo

  • Kujenga vituo vingi vya polisi
  • Mabaraza kufanywa ili kuwashauri wananchi kuepuka maovu/ uhalifu
  • Wageni vijijini kuchunguzwa
  • Hatua kali kuchukuliwa dhidi ya wahalifu
  • Serikali ijishughulishe kumaliza umaskini – kazi kwa vijana/ mikopo ya biashara  
  • Kuimarisha doria wakati wa usiku n.k

Anayekosa kuzingatia sura ya barua rasmi aondolewe maki 4 baada ya kutuzwa  

3.

  • Hii ni insha ya mazungumzo
  • Mtindo uwe wa kitamthilia. Wahusika washiriki moja kwa moja katika mazungumzo kizamu.
  • Majina ya washiriki yaandikwe upande wa kushoto yakifuatwa na koloni (nukta pacha)
  • Maelezo kuhusu vitendo yaweza kuonyeshwa katika mabano.
  • Mtahiniwa aweza kuwapa majina halisi washiriki katika utangulizi
  • Mada ya mazungumzo ni njia za kukomesha uadui unaotokana na ukabila nchini.

Baadhi ya hoja

  • Kuhimiza michezo baina ya makabila  
  • Kazi zibuniwe ili watu wasiwe na nafasi ya kushiriki maovu k.v. vita
  • Ugavi wa raslimali kwa njia ya usawa.  
  • Wahalifu wakamatwe na kufunguliwa mashtaka
  • Nchi iwe na kura/uchaguzi wa haki na huru
  • Viongozi daima wahubiri amani
  • Ndoa baina ya makabila zihimizwe

(Tambua na usahihishe hoja zozote totauti zinazoafikiana na mada)  

  • Asiyezingatia sura ya maznungumzo aondolowe ala.4 baada ya kutuzwa
  • Lazima kila mhusika ashiriki katika mazungumzo

 

4.  Barua hii ni barua rasmi.

  • Iwe na anwani ya mwandishi pembeni kulia.
  • Iwe na anwani ya anayeandikiwa chini kushoto.
  • Barua hii itapitia kwa mwalimu mkuu au mwelekezi wa masomo kabla ya kumfikia mlengwa hivyo itakuwa na anwani mbili.

 

Image From EcoleBooks.comMTINDO

 

 

 

Image From EcoleBooks.com

 

Image From EcoleBooks.com

 

 

Image From EcoleBooks.com

MINT: MWALIKO KATIKA MJADALA

I________________________________________________________________________________

RATIBA

 

SURA

Shule ya upili ya _________________________________________

 

RATIBA YA MJADALA TAREHE 26/02/2010 KATIKA UKUMBI WA MKUTANO WA SHULE

SAA  MAJIRA MATUKIO

9.00 – 9.30 Kuwasili: Kwa wanafunzi na kuingia katika ukumbi

9.30 – 9.35

9.35 – 10.00

– Mwanafunzi aeendeleze katika yake kwa shughuli muhimu za siku hiyo ya mjadala.

Muda mwingi utengewe mjadala wenyewe.

 

5.  (i) Insha ichukue sura ua ripoti.

(ii) Iwe na utangulizi

(iii) Njia za uchunguzi zielezwe

(iv) Sababu za ajali kama :-

  • Ubovu wa barabara nyingi nchini
  • Ubovu wa magari mengi nchini
  • Madereva kutozingatia sheria za barabarani
  • Madereva kutumia mihadarati na kunywa pombe.
  • Abiria kutokuwa waangalifu wanapotumia barabara
  • Madereva ambao hawajahitimu au wasio na ujuzi
  • Askari wa kitengo cha trafiki kula rushwa.

(v) Watoe mapendekezo kama:

  • Barabara zikarabatiwe
  • Magari yakaguliwe mara kwa mara na yaliyo mabovu yasiruhusiwe kutoa huduma barabarani
  • Askari trafiki kuhakikisha kuwa madereva wote wanazingatia sheria za barabarani
  • Madreva walevi na wanaotumia mihadarati kuchukuliwa hatua za kisheria
  • Elimu kupitia vyombo vya habari kwa abiria kuzingatia uslalama wao barabarani
  • Sheria itumike dhidi ya wale wanaoendesha magari na vyombo vya usafiri bila ya leseni.
  • Askari wanaochukua hongo wachukuliwe hatua za kisheria na kinidhamu

(vi) Atoe hitimisho mwafaka

(vi) Aandike jina lake, atie sahihi na kuandika tarehe

 

 

6.  Jibu la swali la kwanza

Sura ya kumbukumbu iwe na :-

  1. Mada/kichwa/anwani
  2. Waliohudhuria
  3. waliotoa udhuru
  4. wasiotoa udhuru
  5. Waalikwa (si lazima)
  6. Ajenda:1. Kusoma na kudhibitisha

    2. Maswali Ibuka

    3. Ajenda 3, 4, 5 n.k ndio maudhui

  7. Kufungua mkutano
  8. Wasilisho la mwenye kiti
  9. maudhui
  10. Shughuli nyinginezo
  11. Kufunga mkutano
  12. Thibitisho

Mwenyekiti sahihi tarehe

………………… ………………..  ………………….

Katibu sahihi tarehe

………………… ………………..  ………………….

Maudhui; Ajenda zitenge:

  • Vijana wapewe mikopo na serikali /benki n.k
  • Vijana waelimishwe ili kuboresha maisha yao
  • Waepukane na kuwa wategemezi
  • Elimu ifanywe ya bure
  • Vijana waelimishwe kutochagua kazi
  • Waepuke uzembe/uvivu
  • Vijana wafunzwe maadili katika jamii ili waepuke ulevi, ukahaba, uvivu na magonjwa kama ukimwi
  • Washiriki siasa ili wahusishwe katika uamuzi na mambo
  • Wamche Mungu
  • Wazame katika ukulima/biashara (hoja zisipungue 5)

UMUHIMU

  • Mtahiniwa ahimize urefu wa insha kuanzia kumbukumbu ya kwanza yaani:

Kumbu 01/10: KUFUNGULIWA KWA MKUTANO

  • asiyetimiza urefu, aondolewe alama 2u

 

7.  Mwanafunzi azingatie vipengele muhimu vya mahojiano kama vile:

 – Hali ya kupokezana mazungumzo kupitia kwa njia ya kuuliza maswali na kutoa majibu

 – Mzungumzaji mmoja asitawale mazungumzo

 – Lugha yenye staha/ adabu

 – Kuwe na mhojiwa (mwanafunzi/ mgonjwa) na mhojiaji (daktari)  

 – Mawazo mazuri yanayofululizwa kimantiki

 

Mambo yafuatayo yanaweza kujitokeza  

 – Maamkizi

 – Sababu za kuja hospitalini

 – Dalili za ugonjwa  

8.  MSAMIATI

Jumla ya maneno yaliyotumiwa kuafikiana na mada au kichwa kilichopendekezwa

MAUDHUI NA MSAMIATI  

baada ya kusoma mtungo utafikiria maudhui na msamiati uliomo kwa jumla

USALAMA ZA KUSAHIHISHA

Hupigwa chini ya sehemu ambaya kosa la sarufi limetokeza kwa mara ya kanza tu.

Hupigwa chini ya sehemu ua neno ambako kosa la hijai limetokeza kwa mara ya kwanza.  

Hutumiwa kuonyesha kuachwa kwa neno

Hutumiwa kuonyesha msamati bora.alama hii hitiwa juu ya neno lenyewe

Hutumiwa kuonyyesha msamiati usiofaa.alam hii hutuwa juu ya neno lenyewe

Maelezo mafupi kuhusu tuzo la mtahini yanahitajika .kila ukurasa uwe na alama ya _chini katikati kuonyesha kuwa mtahini amepitia ukurasa huo  

 

MANENO

maneno  8  –  ukurasa1 ¾

maneno  7  –   kurasa 2

maneno  6  –  kurasa 2 ¼

maneno  5  –  kurasa 2 ¾

maneno  4  –  kurasa3 ¾

maneno  3  –  kurasa4 ½

 

MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

Muundo wa kumbukunbu

i) Kichwa kiwe na mada ,mahali tarehe na saa ya mkutano na kiandikwe kwa herufi kubwa  

ii) Waliohudhuria_itifaki izingatiwe km mkuuu wa wilaya/mwenyekiti.afisa mkuu wa polisi  

,wilayani/katibu.

iii)waliokosa kuhudhuria  

iv) Walioomba radhi/udhuru  

v) Ajenda

vikufunguliwa kwa mkutano  

kumbukumbu zenyewe.orodhesha kumbukumbu kwa majawapo ya mbinu zifuatazo :KUMB.1/2010

KUMB1/7/2010

KUMB.1/26/7/2010 n.k

vii) Shughuli nyinginezo  

ix) Kufungwa kwa mkutano  

x) Thibitisho.mojawapo ya mbinu hizi yaweza kutumiwa

mwenyekiti sahihi tarehe

katibu

au

1. _______________________ 2. ______________________

Mwenyekiti  Katibu  

ii) MAUDHUI

Mtahiniwa agusie mikakati iakayafanywa na kamat ya usalama wilayani kuimarisha usalama wilayani humo k.v.  

a) Hatua kali za ksheria/kinidhamu kuchukuliwa dhidi ya maafisa wa polisi ambao ni wazembe na wafisadi i

b) Ushirikiano kati ya umma na kikosi cha polisi uimarishwe km kuwashirikisha raia

kuwatambua na kuwaripoti wahalifu

c) Nafasi za kazizibuniwe kwa vijana wilayani  

d) Hatua kali zichukuliwe dhidi ya wanasiasa na vyombo vya habari vinavyo chochea wananchi

e) Zawadi zitolewe kwa raia wanaotoa habari kuhusu wahalifu sugu wanao tafutwa na polisi

f) Wahalifu kusakwa na kuchukuliwa hatua kali

g) Maombi ya magari zaidi ya polisi yafanywe kwa serikali kuu  

h) Kushika doria kuimarishwe zaidi  

i) Nambari za dharura za simu zitolewe kwa raia

TANBIHI

Mtahiniwa azingatie sura kamili ya kumbukumbu.anayekosa vipengele viwili au zaidi vya

sura aondolewe 45 (4 Sura)

Mtahiniwa anayekosa kutosheleza urefu aondolewe 2u(2 urefu)  

Urefu unakadiriwa kuwanzia kumbukumbu ya kwanza

 

 

 

9 :SURA

 Hii ni Insha ya mazungumzo

  • -Mtahiniwa anaweza kuandika kichwa au asiandike awashirikishe wote watatu ; mwandishi wa habari aulize maswali na mwenyekiti na Afisa wa sheria wa Tume ya kupambana na ufisadi nchini wajibu
  • Azue maudhui tofauti tofauti ili kuikuza na kuifafanua mada kikiamilifu
  • Atumie nafasi ya 1 na wakati uliopo  
  • Atumie mtindo wa kitamthilia

 

Upungufu ufuatao uadhibiwe

  • Atakayeshirikisha mazungumzo ya mhusika mmoja hadi mwisho halafu wa pili

aongee aondolewe alama 4s (4 sura)  

  • Atakayefanta mhusika mmoja tu aongee bila wa pili kuongea aondolewe 2w(2 wahusika)  .
  • Anayeongezea wahusika wasiokuwepo aondolewe alama 2w (2 wahusika)

 

ii Maudhui- Mbinu kupambana na ufisadi  

  • Kuelimisha wananchi kuhusu madhara ya ufisadi kupitia kwa redio, magazeti,

runinga n.k

  • Ufishaji kupitia kwa redio,magazeti runinga nk
  • Kuwaadhibu wahusika –wapelekwe mahakamani na kufungwa jela.
  • Wananchi wafunzwe maadili
  • Viongozi wawajibike katika kazi zao  
  • Sheri za kupambana na ufishadi zibuniwe na kutekelezwa
  • Kubuni nafasi zaidi za kazi
  • Kuimarisha elimu  
  • Kuongeza mishahara kwa wafanyakazi  
  • Tume zaidi za kukabiliana na ufisadi

 

10.   MUUNDO WA KUMBUKUMBU

  • Kichwa
  • Kumbukumbu za mkutano
  • Tarehe na mahali  
  • Kichwa kiandikwe kwa herufi kubwa na kipigwe mstari  
  • Waliohudhuria  
  • Majina na nyadhifa
  • Wasiohudhuria  
  • Wageni/ waalikwa
  • Ajenda
  • Ufunguzi
  • Mwili – maudhui  
  • Umuhimu wa amani na jinsi ya kuidumisha
  • Mikutano ya mara kwa mara kati ya makabila husika
  • Kuhubiri umuhimu wa kusameheana  
  • Kuhimiza ndoa za mchanganyiko  
  • Viongozi kushurutishwa kutotoa matamshi ya uchochezi
  • Wahalifu kushtakiwa na kuhukumiwa kwa mujibu wa sheria  
  • Washukiwa wakuu wa uchochezi waghasia kushtakiwa na kuhukumiwa kwa mujibu wa sheria
  • Raslimali kugawanya sawa n.k.
  • Shughuli nyinginezo
  • Hitimisho
  • Kufungwa kwa mkutano, saa na maombi
  • Kuthibitishwa  
  • Mwenye kiti  __________ Tarehe ________________  
  • Katibu __________ Tarehe________________  
  • Mtahiniwa azingatie muundo wa kumbukumbu. Asipozingatia sura aondolewe al. 45
  • Mtahiniwa awe ndiye mwandishi wa habari. Asipojihusisha aondolewe alama 2  
  • Mada izingatiwe au asipofanya hivyo atakuwa hajajibu swali

 

11.  Sura ni ya kitamthilia. Kiwe na kichwa, kiwe na utangulizi ukifafanue maudhui na wahusika hasa iwapo mtahiniwa atawapa majina

Wahusika ni mwanahabari na mtahiniwa/ mwanafunzi aliyeibuka bora katika mkoa wa magharibi.

Mwanahabari ndiye atamwuliza mwanafunzi bora maswali naye atamjibu

Maudhui

Miongoni mwa mengine watazungumzia

  1. Mambo yaliyochangia ufanisi wake k.m. bidii, nidhamu, ushuri wa walimu/ wazazi
  2. Himizo kwa wanafunzi wengine
  3. Changamoto alizokumbana nazo katika harakati za maandalizi ya mtihani
  4. Maoni yake kuhusu elimu ya chuo kikuu na kazi ambayo angependa kufanya

Kutuza

Asipojaza urefu aondolewe 24

Akipotoak kisura (asipoandika tamthilia) aondolewe 4

Usemi uwe halisi  

Mkwaju  utumike kwa maudhui

 

12.  Kumbukumbu

Muundo/ umbo/ sura ya kumbukumbu  

a)

  1. Waliohudhuria
  2. Wasiohudhuria na udhuru
  3. Waliokosa kuhudhuria
  4. Wageni/ waalikwa

b) Agenda ya mkutano

  1. Kusomwa kwa kumbukumbu za mkutanouliopita
  2. Yaliyotokana na kumbukumbu za mkutano uliopita  
  3. Matokeo ya mtihani wa 2009
  4. Ulipaji wa karo
  5. Uchaguzi wa waakilishi wa kidato cha kwanza
  6. Namna ya kuwaanda watahiniwa 2010
  7. Miradi ya maendeleo shuleni  
  8. Shughuli nyinginezo
  9. Kufunga mkutano

 

13.  Chanzo cha mzozo:  

  • Uhasama wa kikabila
  • unyakuzi wa ardhi
  • kuzuka kwamaabaka
  • ufisadi
  • wizi wa kura  
  • ubaguzi wa rangi n.k

(b)  Hasara iliyotokana na mzozo:-

  • Majumba yaliyobomolewa
  • watu waliuawa  
  • usafiri ulikataliwa
  • elimu ilizorota  
  • wakimbizi walitokea ikabidi wahudumiwe
  • raslimali zilihabiwa
  • usalama ulizorota  
  • uchumi ulidorora  
  • uhasama wa kikabila uliendelea ziaid

(c)  Namna ya kutatua  

  • kuunda mikakati inayolenga kuwa na uswa wa kijamii  
  • kutoa adhabu kali kwa wanaozua hisia hasi za kikabila  
  • kigawana mamlaka
  • kuunda tuem ya haki na maridhiano  
  • kuanzisha michezo ili kuwepo na mkabala mzuri bain aya jamii

Taz,.(a) Atumie mtindo wa mahojiano –watu wawili au zaidi

-Mpatanishi /msuluhishi na mwanasiasa wadhihike vizuri katika mahojiano

– Mtahiniwa anaweza kuwapa majina lakini aeleze mpatanishi ni yupi na mwanasiasa ni yupi.  

 

14.  Hii ni insha ya ripoti  

 Mtahiniwa azingatie sura ya ripoti

Anaweza kuwa na vijichwa vifuatavyo;  

  • Utangulizi
  • Safari ya kwenda mashindanoni
  • Mashindano yenyewe  

Mbio mbalimbali- Za masafa mafupi/ marefu

Kuruka viunzi

Utupaji wa uzani

Urushaji wa mkuki n.k  

Kilele- mbio za kupokezana vijiti

  • Matokeo ya mashinandano hayo
  • Sherehe ya kufunga mashindano-pengine hotuba mbalimbali kutoka viongozi wa michezo wilayani
  • Hitimisho
  • Kujitambulisha kwa mwandishi- jina na sahihi

Anaweza kuandika kwa mfululizo kiaya huku vijisehemu mbalimbali zikidhihirishwa kwa

mtiririko wenye mantiki inayofaa

Mfuatano wa matukio ujitokeze kwa mtiriririko mzuri. Anayechukua mtindo huu atakuwa

sahihi pia kisura

Asitumie vitambulishi nafsi k.v. ni, tu, n.k.  

Anayetumia vitambulishi nafsi atakuwa na udhaifu wa kimtindo  

 

15.   Insha izingatie mtindo wa barua rasmi

– Anwani mbili

– Mtajo (kwa mhariri)

– Mada

Utangulizi – mwanafunzi aeleze alikotoa habari

Mwili – Mwanafunzi ataje mabadiliko yoyote ya naga k.m kuenea kwa ukama

  • Kuongezeka kwa joto
  • Kupungua kwa mvua
  • Mafuriko

Mwanafunzi aeleze athatri za mabadiliko haya k.m.

  • Kukauka kwa mito
  • Vifo vya wanyama
  • Vifo vya binadamu
  • Kuenea kwa majanga
  • Kuongezeka kwa maji baharini
  • Magonjwa ya ngozi
  • Ukosefu wa chakula

Hitimisho

  • Mwanafunzi atoe njia mwafaka za kukabiliana na mabadiliko ya hali ya anga k.m
  • Kupunguza ukataji wa miti
  • Kupanda miti kwa wingi
  • Kupunguza gesi hatari kutoka viwandani inayoachiliwa hewani

Mwanafunzi ahitimishe kwa kuandika:

  • Jina lake
  • Sahihi
  • Mahali anakotoka


 




Share this:


subscriber

1 Comment

  • Gregory Valentine, January 4, 2024 @ 1:04 pm Reply

    I like this website

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Accept Our Privacy Terms.*